Mahakama
nchini Misri umeamuru kuwa hukumu wa kifo dhidi ya watu 11
waliopatikana na hatia ya kuzua ghasia mbaya wakati wa mechi ya kandanda
miaka mitatu iliyopita itadumu.
Kesi hiyo ilihusu ghasia kati ya
mashabiki hasimu katika kile kiliitwa kuwa mauaji ya halaiki ya uwanja
wa Port Said ambapo zaidi ya watu 70 waliuawa.Maafisa kadha wa polisi walifikishwa mahakamani katika kesi hiyo, lakini hakuna hata moja kati yao aliyehukumiwa kifo. Aliyekuwa mkuu wa usalama katika mji wa Port Said alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.
Polisi walilaumiwa kwa kuwaruhusu mashabiki kutoka timu wenyeji ya al-Masry kuwashambulia mashabiki wa klabu kutoka mjini cairo ya Al-Ahly
No comments:
Post a Comment