Makamu
wa Rais wa zamani wa Shirikisho la Kandanda duniani FIFA Jack Warner
amekumbwa na kashfa ingine na uchunguzi dhidi yake kuhusiana na kupotea
kwa fedha ambazo zililengwa kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa
tetemeko la ardhi lililoikumba Haiti mwaka 2010.
Warner
aliitembelea nchi hiyo miezi kadhaa baada ya tetemeko hilo a kuchangisha
kiasi cha dola dola mia saba na elfu 50 kutoka FIFA na shirika la mpira
wa miguu la Korea kusini kwa ajili ya kuijenga upya nchi hiyo.Lakini hata hivyo, Wachunguzi wa kashfa hiyo rushwa inayoikabili FIFA wanasema fedha hizo zilihamishwa katika Akaunti inayodhibitiwa na Bwana Warner kwa ajili ya matumizi yake binafsi. Miaka minne baadaye fedha hizo bado hazijatolewa maelezo.Warner mwenyewe amekana tuhuma zote zilizotolewa dhidi yake.
No comments:
Post a Comment