GARETH BALE, RAPHAEL VARANE WAICHUNGULIA MANCHESTER UNITED
Leo hii Manchester United imeripotiwa kutoa Ofa ya Pauni Milioni 110 kwa ajili ya Gareth Bale na Raphael Varane. Wawili hao pia wanahusishwa na kuhamia Chelsea. Lakini
kwa mujibu wa Magazeti ya Spain, Cuatro na El Mundo, Real Madrid
imeikataa Ofa hiyo ya Man United ya kuwanunua Bale na Varane ingawa wao
wenyewe wanataka kufanya dili kumchukua Kipa wa Man United David De Gea.huko
Brazil Chombo cha Habari Sambafoot kimedai Man United wako mstari wa
mbele kumnasa Staa mpya wa Timu ya Taifa ya Brazil Roberto Firmino
anaechezea Klabu ya Bundesliga huko Germany, Hoffenheim, kwa Dau la
Pauni Milioni 18. Roberto Firmino nae njiani kutua Man United
No comments:
Post a Comment