Maafisa
wawili wa shirikisho la soka nchini Congo Brazaville wamepigwa marufuku
na shirikisho la soka duniani FIFA kwa ukiukaji wa maadili.
Makamu
wa rais Jean Guy Blaise Mayolas na katibu mkuu Badji Mombo Wantete
hawakubaliwi kushiriki katika maswala yoyote ya soka katika darafa la
kitaifa na kimataifa.Taarifa hiyo iliotolewa na FIFA imesema kuwa uamuzi huo ulichukuliwa baada ya wawili hao kukiuka kanuni na maadili ya FIFA.
Shirikisho hilo hatahivyo halikutoa maelezo zaidi kuhusu hatua yao.
No comments:
Post a Comment