Pages

Tuesday, May 26, 2015

WAMBURA ATANGAZA NEEMA BODI YA LIGI



MKURUGENZI mpya wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Boniface Wambura ameahidi kuzifanyia  kazi  changamoto za ratiba na mapungufu mengine katika kuhakikisha ligi inachezwa kwa ubora msimu ujao.

Wambura aliyasema hayo jana wakati akihojiwa na waandishi wa habari, ikiwa ni siku moja tu tangu  kutangazwa kuchaguliwa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)  kuchukua nafasi   

Alisema suala la ratiba lilikuwa na malalamiko mengi msimu uliopita hivyo katika kuhakikisha hajirudii atahakikisha michuano yote ikiwemo kombe la Mapinduzi, CECAFA, CAF, kalenda ya Fifa,  inaingizwa kwenye ratiba mpya ili kutovuruga utaratibu.

“Tumegundua kuna michezo mingine kama ya Mapinduzi ambayo tulikuwa hatuiweki kwenye ratiba, kuna Cecafa, lakini sasa tutayaingiza ili yasitokee malalamiko mengine,”alisema na kuomba ushirikiano mzuri kwa klabu.

Alisema jambo kubwa lingine ni suala la viwanja kuhakikisha kuwa vinafanyiwa marekebisho hasa ule wa Kambarage kuhimiza vyumba viboreshwe kuepukana malalamiko.

Pia, alisema kupitia mkutano mkuu wa Bodi ya Ligi utakaofanyika hivi karibuni atarajia kufanya mazungumzo na klabu zote kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo kanuni za ligi kwa lengo la kuboresha.

Alisema miongoni mwa changamoto nyingine zilizojitokeza ni baadhi ya timu kuomba kuahirishwa kwa mechi kwani huwa linavuruga ratiba kwa asilimia kubwa.
Wakati huo huo, Uongozi wa Yanga umepongeza uteuzi huo mpya na kuhimiza wachaguliwe wengine watakaoshirikiana na Wmbura katika kusimamia ligi na kuwa bora.

No comments:

Post a Comment