Pages

Tuesday, May 26, 2015

MAPROO WAMIMINIKA JANGWANI KUSAKA NAMBA



WACHEZAJI 12 wa kimataifa wamiminika Jangwani jijini Dar es Salaam  kusaka nafasi ya kuichezea Yanga msimu ujao.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga  jerry Muro alisema kati ya wachezaji hao baadhi wameona wao wenyewe na wengine wamekuja kuomba kusajiliwa Yanga.
“Nia yetu ni kusajili  wachezaji ambao  wana ubora watusaidia kufanya vyema katika michuano ya kimataifa  mwakani, lakini tunaendelea kuangalia kulingana na utaratibu uliowekwa na TFF,”alisema
Alisema ili kupata nafasi ya kuwasajili wachezaji hao wa kimataifa, tayari wamepeleka waraka wa mapendekezo yao Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupendekeza idadi ya usajili kwa wachezaji wa nje ifikie wanane.
Ikiwa watakubaliwa ombi hilo, alisema wataanza mchakato wa kuwasajili wachezaji baadhi ambao wana uwezo wa kusaidia timu hiyo kufanya vyema katika michuano mbalimbali ijayo.
Na ikiwa hawatakubaliwa wataangalia wachezaji watano wazuri na kuwatumia ilimradi wawe na uwezo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Bodi ya Ligi Tanzania Boniface Wambura jana, kila klabu ilipewa taarifa tangu Mei 3, mwaka huu kupendekeza kuhusu kanuni za ligi na idadi ya wachezaji wanaohitajika.
Wambura alisema baada ya mapendekezo hayo yatapitiwa na  Kamati ya Utendaji ya TFF na maamuzi yatatolewa kulingana na kanuni za Shirikisho la Soka duniani (FIFA) na za TFF.
Alisema maamuzi ya mapendekezo ya wachezaji hayo yafanyika mwezi ujao kwani mwisho wa klabu kupelekea mapendekezo yao ni mwishoni mwa mwezi huu.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment