Pages

Tuesday, May 26, 2015

TIDO MHANDO NA WAMBURA WAULA TFF


Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemteua Boniface Wambura kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Bodi ya Ligi Kuu nchini.

Uteuzi huo umefikiwa kwenye kikao cha kamati ya Utendaji ambapo awali kabla ya uteuzi huo atakaoanza kuutumikia rasmi Juni 1 mwaka huu alikuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF.Pia aliwahi kuitumikia TFF kama Afisa Habari wake.

Pia Kamati hiyo ya utendaji imemteau Martin Chacha ambae ni mratibu wa timu za Taifa kukaimu nafasi ya mkurugenzi wa mashindano TFF iliyoachwa na Wambura.

Pia kikao hicho kilifanya mabadiliko na kumteua Leopald Tasso Mkebezi kuwa meneja mpya wa timu ya Taifa.

Mkebezi aliwahi kuwa meneja wa timu hiyo ya Taifa katika kipindi cha miaka sita kuanzia  2006 - 2012.

Pia wajumbe sita waliteuliwa kuongoza Mfuko wa FDF ambao ni sehemu ya utekelezaji wa mapendekezo ya mkutano mkuu wa TFF ulioingiza kipengele cha FDF katika katiba yake.

Mfuko huo utaongozwa Mwenyekiti wake Tido Mhando, ambapo Makamu wake ni Deogratius Lyatto.

Wajumbe ni pamoja na Ephraim Mafuru, Beatrice Singano, Joseph Kahama pamoja na Ayoub Chamshana huku Henry Tandau akiwa ndio katibu mtendaji wa mfuko huo.

No comments:

Post a Comment