Pages

Tuesday, May 26, 2015

TASSO MUKEBEZI ARUDI KUWA MENEJA TAIFA STARS

Kamati ya utendaji ya TFF imesikitishwa na mwenendo mbovu wa Taifa Stars Rais wa TFF, Jamal Malinzi kwa niaba ya kamati ya utendaji amewaomba radhi wapenzi wa mpira kwa matokeo mabaya ya Taifa Stars kwenye michuano ya  Cosafa.

Kikao cha kamati ya utendaji kilipokea taarifa juu ya mwenendo wa timu ya Taifa.

Baada ya majadiliano ya kina, ilikubaliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa, Mart Nooij apewe changamoto maalumu ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN na asipofanikisha jambo hilo mkataba wake utasitishwa mara moja.

Maamuzi haya yamezingatia hali halisi ya timu ya Taifa ambayo inakabiliwa na michuano mbalimbali ya kimataifa ndani ya kipindi kifupi.

Aidha katika kuliimarisha benchi la ufundi la timu ya Taifa, Leopald Tasso Mkebezi ameteuliwa kuwa meneja mpya wa timu ya Taifa.

Mkebezi amewahi kuwa meneja wa timu ya Taifa katika kipindi cha mwaka 2006 - 2012.

No comments:

Post a Comment