LEO
JUMATANO, Februari 25, Uwanja wa Emirates Jijini London utamkumbusha
mbali Meneja wa Arsenal Arsene Wenger wakati watakapoikaribisha AS
Monaco ya France kwenye Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16
ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
AS
Monaco ni Timu ya pili ambayo Wenger alikuwa Meneja wake baada ya
kuanza kazi hiyo Mwaka 1984 huko Klabu ya Nancy-Lorraine Mwaka 1984 na
1987 kuhamia AS Monaco ambako alikaa hadi 1994 na Mwaka uliofuatia
kwenda huko Japan kwenye Klabu ya Nagoya Grampus Eight na kisha kuhamia
Arsenal Mwaka 1996.
Wakati Arsenal ipo Nafasi ya 3 kwenye Ligi Kuu
England nyuma ya Chelsea na Man City, AS Monaco hivi sasa inakamata
Nafasi ya 4 huko Ligi 1 Nchini France ikiwa nyuma ya Olympique de
Marseille, PSG na Olympique de Marseille.
AS
Monaco na Arsenal hazijawahi kukutana lakini Monaco wana Historia nzuri
dhidi ya Klabu za England baada ya Mwaka 1997 kuitoa Newcastle nje ya
UEFA CUP na kutinga Nusu Fainali na 1998 kuitoa Man United toka UEFA
CHAMPIONS LIGI kwenye Raundi kama hii.
Pia Mwaka 2004 walifika Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI baada ya kuibwaga Chelsea kwenye Nusu Fainali.
Lakini
safari hii AS Monaco wana uhaba mkubwa wa Magoli kufuatia kuwatema
Wafungaji wao Radamel Falcao kwa kumpeleka kwa Mkopo Manchester United
na kumuuza James Rodriguez kwa Real Madrid kitu kilichowafanya wafunge
Mabao 25 katika Mechi 26.
Lakini AS Monaco wanae Straika wa zamani
wa Manchester United Dimitar Berbatov, mwenye Miaka 34, ambae licha ya
kufunga Bao 6 tu kwenye Ligi 1 katika Mechi 18, Kocha wa Klabu hiyo,
Leonardo Jardim, amemtaja kuwa ni silaha kubwa kwao kutokana uzoefu na
umahiri wake hasa kwenye Bigi Mechi.
Hata
hivyo, AS Monaco inakutana na Arsenal ambayo kwa Miaka Minne iliyopita
imekuwa ikikwama hatua hii hii ya UEFA CHAMPIONS LIGI kwa mara mbili
kutolewa na Bayern Munich na mara moja moja na Barcelona and AC Milan.
Kila
upande utawakosa Wachezaji kadhaa kutokana na maumivu kwa Arsenal
kutokuwa na Jack Wilshere, Aaron Ramsey, Mikel Arteta, Abou Diaby na
Mathieu Debuchy na Monaco huenda wakamkosa Beki wao wa Kushoto Layvin
Kurzawa na Winga Yannick Ferreira-Carrasco huku Jeremy Toulalan, Tiemou
Bakayoko, Ricardo Carvalho na Andrea Raggi wakiwa nje kabisa.
Mzee Wenger kwenye mazoezi na Vijana wake juu ya Mtanange wa Leo kati yao na Monaco inayocheza League 1

Jembe jipya Paulista

Alex Sanchez

Alex na Theo W.

Kwenye mazoezi

Sanchez kwenye furaha wakati wa mazoezi

Monaco Mjiandaeee!!

Wachezaji wa Arsenal wlipokuwa wanafanya mazoezi kwenye Uwanja wao wa mazoezi Colnel

Leo kwenye Uefa ni sisi na nyie Monaco Emirates
Post a Comment