Pages

Sunday, February 1, 2015

AFCON 2015: CONGO DR YATINGA NUSU FAINALI, YAMYUKA BAO 4-2 JIRANI YAKE CONGO.

Robo Fainali za AFCON 2015, Kombe la Mataifa ya Afrika, zimeanza Leo huko Nchini Equatorial Guinea na Congo DR walitoka nyuma kwa Bao 2-0 na kuwanyuka Jirani zao Congo Bao 4-2 huko Estadio de Bata Mjini Bata Nchini Equatorial Guinea na kutinga Nusu Fainali.
Congo walipata Bao lao la kwanza katika Dakika ya 55 baada ya Frikiki ya Ndinga kuunganishwa na Férébory Dore.
Bao la Pili la Congo lilifungwa Dakika ya 62 kupitia Thievy Bifoum kufuatia makosa ya Kasusula na kumfanya Kipa Kidiaba aokoe Mpira toka kwa Dore lakini ukamrudia Thievy Bifoum aliefunga na kuifanya Gemu iwe Congo 2 Congo DR 0.
Ferebory of Congo celebrates his goal during a quarterfinal match of Africa Cup of Nations between Congo and the Democratic Republic of Congo at the Stadium of Bata, Equatorial Guinea, Jan. 31, 2015. DR Congo won 4-2. (Xinhua/Li Jing)
A football fan of the Democratic Republic of Congo chant before a quarterfinal match of Africa Cup of Nations between Congo and the Democratic Republic of Congo at the Stadium of Bata, Equatorial Guinea, Jan. 31, 2015. DR Congo won 4-2. (Xinhua/Li Jing)
A football fan of the Democratic Republic of Congo chant before a quarterfinal match of Africa Cup of Nations between Congo and the Democratic Republic of Congo at the Stadium of Bata, Equatorial Guinea, Jan. 31, 2015. DR Congo won 4-2. (Xinhua/Li Jing)
Congo DR wakafufuka na kupiga Bao 4 kupitia Mbokani, Dakika ya 65, Loteteka Bokila, Dakika ya 75, Joel Kimwaki, Dakika ya 81, na Mbokani tena Dakika ya 90 na kusonga Nusu Fainali ambapo watacheza na Mshindi kati ya Ivory Coast na Algeria.
Washindi wa Mechi hizo 4 watatinga Nusu Fainali.

No comments:

Post a Comment