Pages

Monday, January 26, 2015

UHAMISHO: SAMUEL ETO'O AFUZU VIPIMO VYA AFYA, ATUA KLABU YA SAMPDORIA.

View image on TwitterStraika wa Everton Samuel Eto'o sasa yupo hatua za mwisho kuhamia huko Italy kwenye Klabu ya Sampdoria baada ya kufuzu upimwaji Afya yake.
Eto'o, mwenye Miaka 33, alijiunga na Everton Agosti 2014 kama Mchezaji huru na kuwafungia Bao 4 hadi sasa.
Hivi sasa Sampdoria wapo Nafasi ya 5 kwenye Ligi ya Serie A wakiwa Pointi 13 nyuma ya Vinara Juventus.
Eto’o, Mchezaji wa Kimataifa wa Cameroun, aliwahi kucheza Serie A akiwa na Inter Milan baada ya kuhamia hapo Julai 2009 na kuifungia Inter Bao 25 katika Misimu yake miwili.
Msimu uliopita, Eto'o, ambae amewahi kuwa Mchezaji Bora Afrika mara 4, alifunga Bao 12 katika Mechi 35 alizoichezea Chelsea aliojiunga nao kwa Mkataba wa Mwaka mmoja akitokea Klabu ya Urusi Anzhi Makhachkala.

No comments:

Post a Comment