Pages

Saturday, January 10, 2015

MATUKIO MBALIMBALI YA MECHI YA YANGA NA JKU KWENYE UWANJA WA AMAAN ZANZIBAR, KOMBE LA MAPINDUZI



FULL TIME 1-0

Mshambuliaji wa timu ya Yanga Kpah Sharman kulia na beki wa timu ya JKU Pansiano Malik wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa robo fainali ya kombe la mapinduzi mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mshambuliaji wa timu ya Yanga Andrey Coutinho, akipiga mpira golini kwa timu ya JKU, katika mchezo wao wa robo fainali uliofanyika uwanja wa Amaan.
Beki wa timu ya JKU, Issa Khaidary,akiondoa mpira huku mshambuliaji wa timu ya Coutinh, akijaribu kunyanganya mpiwa wakati wa mchezo wao wa robo fainali ya kombe la mapinduzi uliofanyika uwanja wa amaan. timu ya JKU imeshinda 1--0.

Mshambuliaji wa timu ya Yanga Kpah Sharman, akimpita beki wa timu ya JKU, Issa Khaidary. ikiwa wanawania kuingia Nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan timu ya JKU imefanikiwa kuingia nusu fainal baada ya kuifunga Yanga bao 1-0
Kikosi cha timu ya JKU kikipasha misuli kabla ya mchezo wao wa Robo Fainal na timu ya Yanga kuaza na kuibuka mshindi kwa kuifunga Yanga bao moja katika kipindi cha pili cha mchezo kupitia mshambuliaji wake Amour Janja.

Kikosi cha timu ya Yanga kikifanya mazoezi mapesimepesi kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa Robo Fainal na timu ya JKU

Rais wa TFF Jamal Malinzi akisalimiana na Kamisaa wa mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Mapinduzi Ndg Mfaume Ali. wakatin wa kuzikagua timu za Yanga na JKU uliofanyika uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Rais wa TFF Ndg. Jamal Malinzi akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Yanga kabla ya mchezo wao wa Robo Fainali na timu ya JKU uliofanyika uwanja wa amaan , timu ya JKU imeshinda bao.
1--0.

Rais wa TFF Jamal Malinzi akisalimiana na wachezaji wa timu ya JKU kabla ya kuaza kwa mchezo wao na timu ya Yanga uliofanyika uwanja wa amaan. Timu ya JKU imeshinda 1--0

Kikosi cha timu ya Yanga kilichokubali kipigo cha bao 1-0, kutoka kwa timu ya JKU, wakati wa mchezo wa nne wa Robo fainali ya Kombe la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa amaan.

Kikosi cha timu ya JKU kilichoitoa timu ya Yanga katika mchezo wa Robo fainali na kuvuka kucheza Nusu fainali na timu ya Mtibwa baada ya kuishinda timu ya Azam kwa matuta mchezo uliofanyika jioni uwanja wa amaan. Mtibwa imeshinda kwa peneti 7-6

No comments:

Post a Comment