Pages

Monday, January 26, 2015

MARIO BALOTELLI NJE NDANI ANFIELD!! KOCHA BRENDAN RODGERS AMSHANGAA MAZOEZINI!!

Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers ametoboa kuwa Straika wa Italy mwenye makeke makubwa Mario Balotelli hajaonyesha kiwango chochote kizuri Mazoezini.
Tangu asainiwe na Liverpool kwa Dau la Pauni Milioni 16 mwanzoni mwa Msimu huu, Balotelli, mwenye Miaka 24, hajafunga Bao hata moja kwenye Mechi za Ligi Kuu England.

Baada ya kumtema kwenye Kikosi kilichotoka 0-0 na Bolton Wanderers hapo Jana kwenye Mechi ya Raundi ya 4 ya FA CUP ambayo Ntaliani huyo alitegenewa kucheza, Brendan Rodgers alisema: “Yeye anajua nini anapaswa kufanya ili awemo kwenye Kikosi.”

Hata hivyo, kurejea kundini kwa Daniel Sturridge, ambae aliifungia Liverpool Bao 28 Msimu uliopita na aliekuwa nje kwa maumivu tangu Agosti, kunamweka Balotelli njia panda hasa baada ya kung’ara na bidii ya Mastraika wengine, Fabio Borini na Rickie Lambert, ambao wote wanagombea Nafasi mbili za Mastraika kwenye Timu. 
Hali hii ya kutupwa nje ya Timu kunazidisha uvumi wa Balotelli kuuzwa kwenye Dirisha la Uhamisho la hii Januari ingawa hadi sasa hakuna hata Klabu inayompapatikia.

No comments:

Post a Comment