Pages

Saturday, January 10, 2015

MAN UNITED & REAL MADRID NDIZO ZENYE UWEZO WA KUMSAJILI LIONEL MESSI

Supa Staa Lionel MessiMENEJA Msaidizi wa Chelsea Steve Holland ametoboa kuwa Klabu yao haina nia kumsaini Mchezaji yeyote Mwezi huu Januari wakati Dirisha la Uhamisho liko wazi na hilo ni hata kama Lionel Messi anapatikana.Lionel Messi celebrates after scoring Barcelona's fourth goal
Zipo habari zinazovuma kuwa Messi yupo kwenye mgogoro na Kocha wa Barca Luis Enrique huku wengine wakivumisha Supastaa huyo wa Argentina atahamia Chelsea lakini Holland amefuta ndoto hiyo.
Holland, akiongea na Wanahabari hii Leo badala ya Meneja Jose Mourinho ‘aliegomea’ baada ya kufunguliwa Mashitaka na FA kwa utovu wa nidhamu, alieleza: “Jose ameshasema wazi Januari haondoki Mtu na wala hatuleti Mtu mpya. Kumsaini Messi ni kitu ambacho hakiwezekani chini ya FFP!”
FFP, Financial Fair Play, ni Kanuni za UEFA zinazotaka kila Klabu ijiendeshe kwa Mapato yake yenyewe bila ruzuku toka kwa Wamiliki wao Matajiri na Klabu ambayo itapata Hasara ya zaidi ya Pauni Milioni 23.5 katika kipindi cha Miaka Mitatu itaadhibiwa na UEFA.

Messi ana Kipengele kwenye Mkataba wake na Barca cha kuruhusiwa kuuzwa kabla Mkataba wake kwisha ikiwa tu Mnunuzi atafikia Dau la Pauni Milioni 196.

Wachambuzi wanadai Klabu pekee Duniani zinazoweza kumudu Dau hilo bila kuvunja Kanuni za FFP kwa sasa ni Man United na Real ingawa watakuwa na mtihani mkubwa kukidhi FFP ukichanganya Maslahi binafsi ya Messi.

Hata hivyo, ikiwa Barca watakubali Dau la kumnunua Messi kulipwa kwa awamu, kitu ambacho inadaiwa Barca hawataki, Klabu nyingine kama vile for Chelsea, Manchester City, PSG na Bayern Munich, zinaweza kumudu kumnunua bila kukiuka FFP.
Lionel Messi akiwa juu juu akipongezwa!

No comments:

Post a Comment