Pages

Friday, January 23, 2015

KLABU YA REAL MADRID NDIO KLABU TAJIRI DUNIANI, IKIFUATIWA NA MANCHESTER UNITED


KWA MIAKA 10 mfululizo, Real Madrid wamekuwa kileleni mwa Listi ya Klabu Tajiri Duniani kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa Jana na Deloitte, ambao ni Wataalam wakubwa wa Mahesabu Duniani.
Manchester United wamepanda kutoka Nafasi ya 4 na kushika Nafasi ya Pili katika Msimamo uliochukulia Mapato ya Mwaka 2013/14 kama ndio kigezo.
Baada ya Man United, Klabu zinazofuatia kwenye Listi hiyo ya Utajiri Duniani ni Bayern Munich, Barcelona na Paris Saint-Germain kisha Klabu za England Manchester City, Chelsea, Arsenal na Liverpool.
Listi hii, ambayo imesheheni Klabu za Ligi kubwa Ulaya, haikuangalia nini Madeni ya Klabu. Ligi hizo 5 kubwa Ulaya ni Ligi Kuu Endland, La Liga ya Spain, Bundesliga ya Germany, Serie A ya Italy na Ligi 1 ya France.

MSIMAMO:
LIGI YA UTAJIRI
1. Real Madrid: 549.5m (518.9m)
2. Man Utd: 518m (423.8m)

3. Bayern Munich: 487.5m (431.2m)
4. Barcelona: 484.6m (482.6m)
5. Paris Saint Germain; 474.2m (398.8m)
6. Manchester City: 414.4m (316.2m)
7. Chelsea: 387.9m (303.4m)
8. Arsenal: 359.3m (284.3)
9. Liverpool: 305.9m (240.6m)
10. Juventus: 279.4m (272.4m)

Premier League clubs' revenues last season

Man UnitedMan CityChelseaArsenal Liverpool Club0100200300400500Millions
Deloitte

No comments:

Post a Comment