Pages

Tuesday, January 6, 2015

KLABU YA BARCELONA YAMFUKUZA MKURUGENZI WAO ANDONI ZUBIZARRETA

Barcelona imemfukuza kazi Andoni Zubizarreta kutoka nafasi yake ya Mkurugenzi wa Soka.
Zubizarreta, mwenye Miaka 53 na Kipa wa zamani wa Barcelona, alichukua wadhifa huo wa Mkurugenzi mwanzoni mwa Msimu Mwaka 2010 baada ya kuondoka kwa Txiki Begiristain ambae sasa yupo Manchester City kama Mkurugenzi wa Soka.

Taarifa ya Klabu ya Barcelona ilisema Rais wao Josep Maria Bartomeu ameamua kuvunja Mkataba na Zubizarreta mara moja.

Zubizarreta alikuwa Kipa wa Barca kati ya Miaka 1986 na 1994 na pia kuidakia Spain mara 126.

Huko Spain Wadau wengi wamekuwa wakimlaumu Zubizarreta, ambae alihusika na Uhamisho wa Wachezaji, kwa janga la kufungiwa na FIFA kuuza na kusajili Wachezaji wapya kwa Mwaka huu wote kutokana na kukiuka Kanuni za Kusajili Wachezaji Chipukizi wa chini ya Miaka 18 kutoka nje ya Spain.
Zubizarreta aliusika kwenye usajili wa  Thomas Vermaelen ambaye mpaka sasa anaendelea kukipiga na Klabu hiyo ya Barca.

Kipa Marc Andre ter Stegen alisajiliwa  akitolewa  Borussia Monchengladbach 

No comments:

Post a Comment