Pages

Saturday, January 24, 2015

ILALA YAJINAFASI KULIBAKISHA KOMBE LA TAIFA CUP DAR ES SALAAM





UONGOZI wa Mkoa wa Soka wa Ilala, umesema kitendo cha timu ya wanawake “Ilala Queens” kutinga robo fainali ya mashindano ya Taifa Cup si cha kubahatisha.

Akizungumza jijini Katibu wa Chama cha Soka Mkoa wa Ilala, Daud Kanuti amesema Ilala wana wachezaji wazuri wenye kila sababu ya kutwaa ubingwa wa Taifa Cup na kuwaomba wadau kuwapa sapoti.

“Ilala kuingia robo fainali si kwamba tulibahatisha bali ni mbio za kuelekea nusu fainali na baadae na kulibakisha kombe ndani ya jiji la Dar es Salaam kwani itakuwa aibu Dar es Salaam tuwe wanzishilishi wa ligi ya wanawake halafu kombe liende mikoani”, alisema Kanuti.

Ilala imefuzu robo fainali baada ya kuifunga Mtwara queens mabao 5-0 kwenye uwanja wa Karume na baadae kwenda kurudiana nao kwenye Uwanja wa Nang’wanda Sijaona, Mtwara na kufungwa bao 1-0.

Mikoa mingine iliyofuzu kwenye robo fainali inayotarajiwa kuanza kesho ni Kigoma, Mwanza, Pwani, Tanga, Temeke,  Iringa na Mbeya na timu hizi zitawasili jijini leo.

Taifa cup ya wanawake ni mashindano ya kwanza kufanyika nchini na yanadhaminiwa na kampuni ya Proin na imeshirikisha mikoa yote mwanachama wa TFF.

No comments:

Post a Comment