Pages

Thursday, January 8, 2015

FUNUNU ZAWACHANGANYA MASTAA BARCELONA, LIONEL MESSI KUTAKA KUTIMKIA CHELSEA.

WACHEZAJI WAKUBWA wa Barcelona wamefanya Kikao cha dharura na Staa wao mkubwa Lionel Messi huku kukiwa na uvumi mkubwa kuwa Muargentina huyo huenda akatimkia Chelsea.
Zipo ripoti kuwa Messi amegombana na Kocha wa Barcelona, Luis Enrique, na hivyo hana furaha huko Nou Camp.

Hata hivyo, hii Leo Luis Enrique amekataa kuzungumza lolote kuhusu bifu lake na Messi huku aking’ang’ania kuwa yale yanayoongelewa ndani ya Chumba cha Kubadili Jezi hubaki humo humo.

Lakini Wachezaji Wakongwe wa Barca, wakiongozwa na Xavi, hii Leo kabla ya Mazoezi yao, walifanya Kikao na Messi, mwenye Umri wa Miaka 27.
Inadaiwa kuwa Messi amechukizwa na uongozi wa Enrique na pia kupigwa Benchi Jumapili iliyopita wakati Barca inachapwa 1-0 na Real Sociedad.
Akiwa chini ya Mameneja waliopita wa Barca, kina Pep Guardiola, Gerardo Martino na Tito Vilanova, Messi alikuwa akicheza karibu kila Mechi.
Inasemekana kutoelewana kati ya Messi na Enrique kulilipuka Ijumaa iliyopita na nusura wawili hao wakamatane wakati wa Mazoezi.

Juzi Jumatatu Messi hakuhudhuria Mazoezi na Klabu haraka haraka kutangaza alikuwa Mgonjwa akiumwa Tumbo lakini Siku hiyo hiyo Messi akaanza kuifuatilia Chelsea kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram na kulipua dhana kuwa yu njiani kutua Stamford Bridge.
Huku pia kukiwa na uvumi kuwa Luis Enrique atatimuliwa, mwenyewe ameeleza: "Sitaki kuzungumza lolote. Tunajua vitu hubadilika na Mwezi mmoja ni mrefu sana. Bado nina furaha hapa.”
Kisha akaongeza: “Ni vitu vya kupinga tu, hamna ukweli. Sidhani natakiwa kukubali au kukataa uvumi huu. Hiyo italeta matatizo zaidi badala ya kuondoa.”

Hata hivyo, huko Spain kunazizima hasa baada ya kujulikana kuwa Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu, ataongea na Wanahabari baadae hii Leo.
 

Barcelona wamewakanya Chelsea kuwa Kijana wao hauzwi na wala hatoki  Nou Camp

Messi alianzia benchi mechi ya Real Sociedad na hapa ndipo fukuto na ubaya ulianzia kwa upande wake na kocha Luis Enrique

Enrique  ameonekana kuchanganyikiwa kutokana na kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Sociedad

Rais wa Barcelona  Josep Bartomeu  kulizungumzia hili kati ya Kocha na Messi.

Meneja wa Barcelona Enrique kumbakisha Messi Klabuni Nou Camp

Enrique kwenye Ukumbi wa Habari

No comments:

Post a Comment