Pages

Saturday, January 24, 2015

CHELSEA SOKONI KUMTAFUTA JUAN CUADRADO NA DOUGLAS COSTA, ANDRE SCHÜRRLE NA MOHAMED SALAH KURUDISHWA SOKONI

Chelsea, wako mbioni kuwatema Mohamed Salah na André Schürrle ili kumnasa Kiungo wa Klabu ya Italy Fiorentina, Juan Cuadrado, anaetoka Colombia na Douglas Costa.
Mohamed Salah, Mchezaji wa Miaka 22 kutoka Egypt, alinunuliwa na Chelsea kutoka FC Basel ya Uswisi Mwaka mmoja uliopita na amecheza Mechi 6 tu za Ligi Kuu England na Msimu huu amecheza Dakika 30 tu za Mechi kubwa kwa Klabu yake.
Hata hivyo Uhamisho wa Salah sasa umegubikwa na utata baada kutokea mvutano kati ya Mchezaji huyo na Wakala, Oliver Kronenberg, ambae ndie alimhamisha Mmisri huyo Stamford Bridge.
Mbali ya Salah, Chelsea watalazimika kumuuza André Schürrle ili kufanikisha azma yao ya kumnunua Juan Cuadrado kutoka Fiorentina ambao wanataka si chini ya Pauni Milioni 26.8 ili kukidhi Kipengele cha Mkataba cha kumuuza Mcolombia huyo.

Hivi sasa Mjerumani Schürrle anawaniwa na Klabu za Nchini kwao Wolfsburg na Borussia Dortmund.

No comments:

Post a Comment