Pages

Thursday, December 11, 2014

SAMIR NASRI na ZABALETA WAIPA USHINDI CITY IKIIFUNGA AS ROMA 2-0 UEFA CHAMPIONS LEAGUE

Samir Nasri akishangilia bao lake la kwanza dakika ya 60 kipindi cha kwanza baada ya kumaliza kipindi cha kwanza bila bao.Dakika ya 60 Samir Nasri aliachia shuti kali lililogonga posti na kuzama ndani ya nyavu na kuipa bao City 1-0 dhidi ya As Roma kwenye Uwanja wao Stadio Olimpico, Roma Mwamuzi akiwa ni M. Mažić baada ya kupata pasi kutoka kwa Gael Clichy. Bao hilo lilifanya As Roma sasa waweze kutafuta bao mbili tena. 

Bao la pili la Man City lilifungwa dakika za majeruhi dakika ya 86 na Pablo Zabaleta baada ya kupewa pasi na Samir Nasri.Kipindi pande zote mbili zilikuwa ngumu kufungika!Kipindi cha kwanza kikiendelea..Mabingwa wa England, Manchester City, watatinga kwenye Mechi yao ya mwisho ya Kundi E la UEFA CHAMPIONS Ugenini huko Mjini Rome, Italy kucheza na AS Roma wakihitaji kushinda na pia miujiza mingine ili wafuzu kwenda Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Kwenye Kundi E tayari Bayern Munich wameshafuzu na kuacha kinyang’anyiro cha Timu ipi itaungana nayo kwa Timu 3 zilizobakia ambazo ni AS Roma, Man City na CSKA Moscow.
Timu zote hizo 3 zina Pointi 5 kila mmoja lakini nani ataungana na Bayern ni kitendawili kikubwa hasa ukichukulia Kanuni za UEFA hupima matokeo ya Uso kwa Uso kwa Timu zilizofungana Pointi.
Kati ya Timu hizo 3 hatima ya AS Roma iko mikononi mwao wenyewe kwani wakiifunga City wao watafuzu.
AS Roma wakitoka Droo na City inaweza ikawasaidia na pia inaweza ikawaua ikitegemea CSKA wamefanya nini kwenye Mechi yao Mjini Munich na Bayern Munich.
CSKA wao wanaweza kufuzu ikiwa wataifunga Bayern huku AS Roma ikishindwa kuifunga City.
City watafuzu wakiifunga Roma na CSKA kutoshinda.
Lakini Mahesabu yatakuwa magumu pale Mechi ya City na Roma kuwa Sare.

RATIBA
Jumatano Desemba 10
KUNDI E

Bayern Munich vs CSKA Moscow
AS Roma vs Man City

KUNDI F
Ajax v Apoel Nicosia
Barcelona v Paris Saint Germaine

KUNDI G
Chelsea v Sporting Lisbon
NK Maribor v Schalke

KUNDI H
Athletic Bilbao v BATE Borisov
FC Porto v Shakhtar Donetsk

No comments:

Post a Comment