Pages

Saturday, December 13, 2014

PARDEW MENEJA BORA NA MCHEZAJI WA CITY SERGIO AGUERO

MENEJA wa Newcastle Alan Pardew ndie ameteuliwa Meneja Bora wa Ligi Kuu England kwa Mwezi Novemba na Mchezaji Bora ni Sergio Aguero wa Manchester City. 

Alan Pardew, mwenye Miaka 53, alishinda Mechi 3 kati ya 4 na kuwabwaga Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, na Manuel Pellegrini wa Man City ambao hawakufungwa hata Mechi moja. 
Hivyo hivyo, Sergio Aguero amepewa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi wakati Mchezaji wa QPR, Charlie Austin, na wa Burnley Danny Ings walifunga Bao 3 kama Aguero ambae hii itakuwa Tuzo yake ya Pili.

No comments:

Post a Comment