Pages

Tuesday, December 30, 2014

MWAMUZI ALIYECHEZESHA MTANI JEMBE AZAWADIWA BEJI YA FIFA



 
Mwamuzi Jonesia Lukyaa (wa tatu toka kushoto) akiwa na wenzake kabla mchezo wa mtani jembe
MWAMUZI wa aliyechezesha mechi ya mtani jembe, Jonesia Rukyaa amepata beji ya FIFA na waamuzi wengine wa kike sita.
 
Jonesia ambaye alimudu vema kuchezesha mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa Desemba 13, mwaka huu na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga amepata beji hiyo na Florentina Zablon toka Dodoma na Sophia Ismail toka Mara kama waamuzi wa kati huku waamuzi wasaidizi wakiwa ni Hellen Mduma wa Dar es Salaam, Kudra Omary toka Tanga, Grace Wamala toka Kagera na Dalila Jaffary toka Zanzibar.

Katika taarifa ambayo imeweka kwenye blogu http://refereesfifa.blogspot.com inasema kuwa Israel Mujuni wa Dar es Salaam, Waziri Sheha wa Zanzibar, Martin Saanya wa Morogoro na Mfaume Nassoro wa Zanzibar wamepata beji hizo kama waamuzi wa kati huku Samwel Mpenzu wa Arusha, John Kanyenye wa Mbeya, Frednand Chacha wa Mwanza, Josephat Bulali wa Dar es Salaam, Sudi Lila na Frank Komba wa Pwani wakipata beji hizo kama waamuzi wasaidizi.

Tanzania imepata beji nyingi za FIFA kwa upande wanawake msimu huu wa 2015 kwani haijawahi kupata beji zaidi ya nne kuanzia ianze kutoa waamuzi wa kike kwani hata mwaka huu haikuwa na mwamuzi mwenye beji wa kike.

Waamuzi wa kike ambao walishawahi kuwa na beji za FIFA ni kuanzia 2006 ni Flora Kashaija, Isabela Kapera na Judy Gamba kama waamuzi wa kati na waamuzi wasaidizi ni Zahara Mohamed, Saada Tibabimale, Mwahija Omary toka Zanzibar.

Katika historia ya soka la Tanzania huwezi kuacha kumtaja Elizabeth Kalinga toka Mbeya lakini hakubahatika kupata beji ya FIFA kwani umri wake ulikuwa umepita wakati FIFA ilipoanza kutoa beji hizo kwa Tanzania

No comments:

Post a Comment