Pages

Wednesday, December 31, 2014

KOCHA ALAN IRVINE WA WEST BROM ALBION ATIMULIWA

Meneja Alan Irvine afukuzwa West Bromwich Albion
Alan Irvine ametimuliwa kama Meneja wa West Bromwich Albion baada ya kudumu kwa Miezi 7.
Irvine, mwenye Miaka 56, aliteuliwa Mwezi Juni kumrithi Pepe Mel na kupewa Mkataba wa Mwaka mmoja ambao ungeweza kuongezwa.

Hivi sasa WBA wapo Nafasi ya 16 kwenye Msimamo wa Ligi Kuu England­­­­­ wakiwa Pointi 1 tu juu ya zile Timu 3 ambazo zipo eneo hatari la kushuka Daraja baada ya Jumapili kuchapwa 2-0 na Stoke City kikiwa ni kipigo chao cha 7 katika Mechi 9. Mechi inayofuata kwa WBA ni hapo Alhamisi Januari Mosi ambapo watacheza Ugenini na West Ham na Timu hiyo itakuwa chini ya Makocha Wasaidizi Rob Kelly akisaidiwa na Keith Downing.
Hivi Juzi Crystal Palace ilimtimua Meneja wao Neil Warnock na kumfanya awe Meneja wa kwanza kuondolewa Msimu huu na sasa amefuatia Irvine.
KAPUNOVIC ATUA TAYARI KUINOA SIMBA. HATIMAYE kocha mpya wa klabu ya Simba, Goran Kopunovic raia wa Serbia amewasili jijini Dar es Salaam leo asubuhi huku akitamba kuwa anaifahamu yanga vizuri. Akihojiwa na blog ya Bin Zubeiry, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa, Dar es Salaam, kocha huyo kijana amesema mafurahi kuja kuinoa Simba kwani ni klabu kubwa na amepania kuiletea mafanikio. Kapunovic amesema anatarajia kukutana na uongozi wa Simba kwa mazungumzo na kusaini mkataba na baada ya hapo ataanza kazi rasmi. Akizungumzia kuhusu wapinzani wa jadi, Yanga SC, Kopunovic amesema kwamba anawajua vizuri na anafahamu kuhusu soka ya Tanzania kwa ujumla. Kapunovic anakuja baada ya kutimuliwa kwa kocha Patric Phiri kutoka Zambia kutokana na matokeo yasiyoridhisha ya timu hiyo kikiwemo kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Kagera Sugar.

Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win

No comments:

Post a Comment