Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, October 7, 2014

Wanyarwanda kuchezesha mechi ya Stars na Benin



taifa stars 2014

Waamuzi kutoka Rwanda ndiyo watakaochezesha mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kati ya Taifa Stars na Benin itakayofanyika Jumapili (Oktoba 12 mwaka huu) jijini Dar es Salaam. Hakizimana Louis ndiye atakayeongoza waamuzi hao wa FIFA kwa kupuliza filimbi kwenye mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 jioni. Atasaidiwa na Simba Honore na Niyitegeka Jean Bosco.
Mechi hiyo itatanguliwa na ile ya viongozi wa dini- Kiislamu vs Kikristo kudumumisha upendo, amani na ushirikiano itakayoanza saa 9 kamili alasiri. Tiketi za elektroniki zitakazotumika kwa mechi hiyo tayari zimeanza kuuzwa kwa kiingilio cha sh. 4,000 na sh. 10,000.

No comments:

Post a Comment