Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, October 7, 2014

CAF YAITOSA TANZANIA KUWA MWENYEJI AFCON 2017, YATOA SABABU


RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI (KUSHOTO) AKIWA NA RAIS WA CAF, ISSA HAYATOU.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limefahamishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuwa Tanzania haitaweza kuwa mwenyeji wa Fainali za Afrika- AFCON 2017 kwa kuwa haijawahi kuandaa fainali zozote za vijana Afrika. Fainali hizo ni zile za vijana wenye umri chini ya miaka 17 na 20.

Hivyo, TFF inaelekeza nguvu zote katika kuandaa Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka U17 mwaka 2019.
Tunapenda kuchukua fursa hii kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazania, Jakaya Kikwete kwa kututia moyo katika kuomba uenyeji wa AFCON 2017.
Pia tunamshukuru Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara kwa juhudi binafsi alizozionyesha katika jitihada za Tanzania kuomba uenyeji  wa AFCON 2017.

TFF inaamini kwa dhati kuwa uenyeji wa Afrika U17 2019 utaifungulia Tanzania milango ya kuandaa mashindano makubwa zaidi.


Kwa hisani ya Saleh Jembe blog

No comments:

Post a Comment