![]() |
Arsene Wenger akimsukuma Jose Mourinho kifuani kunako dakika ya 20 katika mchezo uliopigwa darajani Stamford Bridge Jumapili ya leo |
Upinzani
baina ya Arsene
Wenger na Jose Mourinho umechukua sura mpya katika dimba la Stamford
Bridge Jumapili ya leo baada ta meneja wa Arsenal kumsukuma mwenzake
licha ya kuamuliwa na hali ya mambo kurejeshwa katika usalama bado
wawili hao walishindwa kupeana mikono baada ya filimbi ya mwisho ya
mchezo huo.
tukio
hilo lilitokea kufuatia Wenger
kukasirishwa na kitendo cha Gary Cahill kumkabili visivyo mshambuliaji
wake Alexis Sanchez kunako dakika ya 20 ambapo mlinzi huyo wa Chelsea
alizawadiwa kadi ya njano na mwamuzi kwa kile kilichoonekana alikuwa
amefanya madhambi makubwa.
Meneja
mfaransa Wenger kwa hamaki kubwa aliondoka katika eneo lake la ufundi
la kumdhihaki mwamuzi wa mchezo huo Martin Atkinson na kisha kumuonyesha
mkono wa dharau meneja wa Chelsea Mourinho aliyekuwa anaelekea upande
wake.
Wenger akibwatukiana na meneja wa Chelsea Mourinho darajani
Wawili
hao walitenganishwa na mwamuzi wa akiba Jonathan Moss wakati
makabiliano yalipojitokeza tena hii leo Daraji Stamford Bridge( tumia
neno 'dugout')
Wenger mwenye umri wa miaka 64, alimsukuma Mourinho kifuani huku meneja wa Chelsea Mourinho ambaye ni mdogo wa kwa miaka 13
nyuma ya Wenger.
Meneja
huyo wa Arsenal baadaye aligeuka na kutaka kuondoka kabla ya kurejea
tena akiwa ameweka mikono mfukoni na kuanza kubwatukiana kama mnyama
mbwa kimya kimya dhidi ya Mourinho.
Atkinson
aliwaita wote wawili na kuwadokezea kuwa endapo wataendelea na sakata lao la aibu kubwa uwanjani basi atawapeleka jukwaani.
Wenger
na Mourinho waliendelea kubadilishana matusi hata baada ya
kutenganishwa karibu sehemu yote ya mchezo iliyosalia katika kipindi cha
kwanza huku meneja msaidizi wa Chelsea Rui Faria na yule wa Arsenal
Steve
Bould wakionekana kuingilia ugomvi wa wakubwa wao wa kazi.
Ndani
ya uwanja matokeo haya yanakuwa ni kama aibu kubwa kwa Wenger, ambaye
hayajawahi kumfunga Mourinho katika jumla ya michezo 11 iliyopita huku
Eden Hazard akifunga goli kwa njia ya penati baada ya kufanyiwa madhambi
na Laurent Koscielny ndani ya sanduku la hatari na kuwapa wenyeji
Chelsea goli la kuongoza.
Bao
la pili la washindi lilitiwa nyavuni na Diego Costa kunako dakika ya 78
ya mchezo likiwa ni goli la tisa kwa mshambuliaji huyo msimu huu wa
ligi.
Mwamuzi
Mark Atkinson akiwaita mabosi hao kufuatia tukio la aibu uwanjani na
kutishia kuwaondoa katika eneo la ufundi na kuwapeleka jukwaani
Wenger alikasirishwa na rafu mbaya aliyofanyiwa mshambuliaji wake Alex Sanchez na Gary Cahill kunako dakika ya 20 ya mchezo.
No comments:
Post a Comment