Pages

Tuesday, September 2, 2014

WENGER ATIMKIA ITALIA KWENDA KUCHEZESHA MECHI YA HISANI WAKATI WENZAKE WAKIHAHA NA USAJILI WA DAKIKA ZA MWISHO


WAKATI hekaheka za usajili zikiendelea kushika kasi katika kipindi hiki cha mwisho, meneja wa Arsenal Arsene Wenger yeye atatumia muda huu wa saa chache uliobakia kabla ya dirisha la usajili kufungwa jijini Rome akiwa kama mwamuzi wa mechi hisani. 

Mfaransa huyop alisafiri kwenda Italia kwa ajili ya mechi iliyoandaliwa maalumu kuhamasisha amani itakayofanyika katika Uwanja wa Olimpiki ambapo baadhi ya nyota kama Andrea Pirlo, Samuel Eto’o, Ronaldinho, Gianluigi Buffon, Diego Maradona, Paulo Maldini na Andriy Schevchenko watakuwwepo katika mchezo huo. 

Chanzo kimoja cha habari kutoka ndani ya klabu hiyo kimesisitiza kuwa kutokuwepo kwa Wenger hakutaathiri kwa vyovyote uwezo wao wa kusajili katika muda wa mwisho. 

Hata hivyo inafahamika kuwa katika muda huu wa mwisho Arsenal wametupa ndoano yao kwa Matija Nastasic, Weinston Reid na Ron Vlaar ili mmoja wao aje azibe nafasi ya Thomas Vermaelen. 

Kwa upande wa ushambuliaji Wenger anaonekana kama ameridhika na aliokuwa nao pamoja na kuumia kwa Olivier Giroud baada ya kuwakosa Loic Remy aliyekwenda Chelsea na Radamel Falcao aliyekwenda Manchester United kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Kuna uwezekano wa Arsenal kusajili mchezaji mmoja au wawili kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili lakini haidhaniwi kama atasajili mshambuliaji tena pamoja na upungufu aliokuwa nao katika safu hiyo.

No comments:

Post a Comment