Pages

Tuesday, September 2, 2014

VIZA YAMCHELEWESHA MARCOS ROJO KUICHEZEA MANCHESTER UNITED

MCHEZAJI mpya wa Manchester United Marcos Rojo amechelewa kuanza kuichezea Timu yake kutokana na kutopewa Viza ya kufanya kazi Nchini Uingereza.
Imeripotiwa kuwa kuchelewa kupewa Viza hiyo ya Kazi kunatokana na kukabiliwa na Kesi huko Nchini kwao Argentina ya kugombana na Jirani yake Mwaka 2010.
Awali ilidhaniwa kuwa Rojo, ambae amehamia Man United kutoka Sporting Lisbon ya Ureno Siku 11 zilizopita, kulitokana na Umiliki wa Haki za Biashara za Mchezaji huyo kuwa chini ya pande mbili lakini sasa FA, Chama cha Soka England, kimetoboa kuwa Mchezaji huyo ashapewa Hati ya Kimataifa ya Uhamisho na wao kumruhusu kuichezea Man United.
Meneja wa Man United, Louis van Gaal, amesema ana hakika Mchezaji huyo ataichezea Man United Mechi inayofuata ya Ligi hapo Septemba 14 na QPR Uwanjani Old Trafford.
Ligi Kuu England, baada ya Mechi za Wikiendi hii, itasimama kupisha Mechi za Kimataifa hadi Septemba 13.
Rojo alipokwenda Jijini Manchester kukamilisha taratibu zake za Uhamisho aliruhusiwa kuingia Nchini humo kwa Viza ya Kitalii.
Mwanasheria wa Rojo huko Argentina, Fernando Burlando, amesema Kesi ya Rojo inangoja kusikilizwa lakini itamalizika muda wowote lakini amesema hata akipatikana na Hatia Adhabu atakayopewa itakuwa Kifungo cha Nje na kuitumikia Jamii bure na zote hizo zinaweza kufanywa nje ya Nchi.

RATIBA:LIGI KUU ENGLAND
Jumapili Agosti 31
15:30 Aston Villa v Hull
15:30 Tottenham v Liverpool
18:00 Leicester v Arsenal

Jumamosi Septemba 13
14:45 Arsenal v Man City
17:00 Chelsea v Swansea
17:00 Crystal Palace v Burnley
17:00 Southampton v Newcastle
17:00 Stoke v Leicester
17:00 Sunderland v Tottenham
17:00 West Brom v Everton
19:30 Liverpool v Aston Villa

Jumapili Septemba 14
18:00 Man United v QPR
Jumatatu Septemba 15
22:00 Hull v West Ham

No comments:

Post a Comment