Pages

Tuesday, September 2, 2014

Falcao atua United dakika za majeruhi kumsaidia Van Persie




Ikiwa leo ni siku ya mwisho ya kusajili wachezaji wapya katika vilabu vya soka nchini barani Ulaya.
Klabu ya Manchester United imekamilisha usajili wake kwa kumsajili Radamel Falcao ambaye amejiunga kwa mkopo wa msimu mzima.
Falcao alijiunga na Monaco kwa dau la dola milioni hamsini mwaka 2013.
Baadhi waliona taarifa hizo kama fununu tu.
Bila shaka usajili wa Falcao katika Manchester United unaonekana kama mapinduzi kwani vilabu vingi vilikuwa vimemuotea Falcao ambaye anachezea klabu ya Ufaransa ya Monaco.
Falcao ameifungia Monaco jumla ya mabao 11 akicheza michezo 20. Mkataba huo unaipa fursa Manchester United kumnunua mchezaji huyo kwa pauni milioni 43.5 mwishoni wa kipindi cha mkopo.
Klabu ya Louis van Gaal ambayo kama vilabu vingine Ulaya vilifahamu tu kumhusu mchezaji huyo na uwezo wa kununua katika dakika za mwisho mwisho.
Wakati huohuo, Manchester United itaikopesha Real Madrid mchezaji wake nyota Javier Hernandez.
 Familiar face: Falcao was part of the Monaco side that played Arsenal in the Emirates Cup in pre-season

klabu alizopitia Falcao idadi ya michezi(apps) na magoli aliyofunga(goals)

River Plate (2005-09): 105 apps/45 goals
Porto (2009-12): 87 apps/72 goals
Atletico Madrid (2011-13): 91 apps/70 goals
Monaco (2013-14): 22 apps/13 goals
Colombia: 51 caps/20 goals
Mshambuliaji huyu alikuwa akihusishwa na kuelekea Manchester City katika siku ya mwisho ambapo pia Arsenal wiki iliyopita walijaribu kujiunga na mbio hizo.
Lakini United ikatupia chambo bora katika ndoano na kufanikiwa kupata saini yake ambapo sasa hofu ya majeruhi ya Robin van Persie haitakuwa na wasiwasi mkubwa huku pia wakiwa wanaelekea kumuuza Danny Welbeck na Javier Hernandez ambaye amejiunga na Real Madrid.

No comments:

Post a Comment