Pages

Friday, September 5, 2014

SIR ALEX FERGUSON AONGOZA MKUTANO WA MWAKA WA MAKOCHA, VAN GAAL AKWEPA

Sir Alex Ferguson akizungumza na Carlo Ancelotti na Arsene Wenger katika mkutano wa makocha mjini Nyon MKUTANO wa mwaka wa makocha wa kiwango cha juu umeanza jana jumatano na kumalizika leo, makao makuu ya UEFA, mjini Nyon, Uswizi.
Kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson alikuwa mwenyekiti wa mkutano huo akiwa kama balozi wa makocha wa UEFA , wakati naye Rais Michele Platini alikuwepo. Ferguson alinaswa na kamera akitaniana na aliyekuwa mpinzani wake mkubwa Arsene Wenger, wakati bosi wa Manchester City, Manuel Pellegrini naye alikuwepo katika tukio hilo. Wakizungumzia mchezo mzuri: Rais wa UEFA Michele Platini akizungumza na Ancelotti na Ferguson leo alhamisi. Picha ya pamoja ya makocha katika makao makuu ya UEFA leo nchini Uswizi. Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho akiwa amekaa na kocha wa zamani wa Stamford Bridge, Carlo Ancelotti
Mourinho akizungumza na waandishi wa habari nje ya makao makuu ya UEFA leo.

Hata hivyo, kocha wa mashetani wekundu, Manchester United, Louis van Gaal - ambaye ni mshindi wa Bundesliga, La Liga na Eredivisie - hakuwepo katika mkutano huo kwasababu timu yake haishiriki michuano ya UEFA mwaka huu.

Louis van Gaal hakuhudhuria mkutano huo.

MAKOCHA WALIOHUDHURIA MKUTANO WA MAKOCHA MWAKA 2014 MAKAO MAKUU YA UEFA NI:-

Michele Platini - UEFA President
Sir Alex Ferguson
Gianni Infantino - UEFA General Secretary
Ioan Lupescu - UEFA Chief Technical Officer
Giorgio Marchetti - UEFA Competition Director
Pierluigi Collina - UEFA Chief Refereeing Officer
Laurent Blanc - PSG manager
Manuel Pellegrini - Man City manager
Nuno Espirito Santo - Valencia manager
Jens Keller - Schalke manager
Mircea Lucescu - Shakhtar Donetsk manager
Jorge Jesus - Benfica manager
Unai Emery - Valencia manager
Jurgen Klopp - Borussia Dortmund manager
Roger Schmidt - Bayer Leverkusen manager
Andre Villas-Boas - Zenit St Petersburg manager
Miguel - Olympiakos manager
Rafael Benitez - Napoli manager
Carlo Ancelotti - Real Madrid manager
Pep Guardiola - Bayern Munich manager
Luis Enrique - Barcelona manager
Arsene Wenger - Arsenal manager

No comments:

Post a Comment