Pages

Friday, September 5, 2014

CRISTIANO RONALDO AJISAFISHIA NJIA KURUDI OLD TRAFFORD.

MCHAMBUZI na Mtaalam wa Soka la Spain, Paul Breen-Turner, anaamini Staa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo anajisafishia njia ya kurudi Klabu yake ya zamani Manchester United.
Ronaldo, ambae ndie Mchezaji Bora Duniani, aliihama Man United Mwaka 2009 na kujiunga na Real Madrid lakini Siku zote amekataa kukanusha kwamba hatarudi Old Trafford ambako ndiko Ustaa wake ulichipukia.

Breen-Turner amedai hivi sasa Ronaldo amekerwa na Sera ya kuuza Wachezaji ya Real ambako hivi karibuni walimuuza Angel Di Maria huko Man United kwa Dau la Rekodi ya Uingereza na pia Xabi Alonso kwenda Bayern Munich.
Mchambuzi huyo amesema: “Hivi karibuni alihojiwa na Wanahabari na kutamka: ‘Ningekuwa nashughulikia Uhamisho, nisingefanya vitu namna hii kama walivyofanya!’ Na kauli hii imemuudhi Rais wa Real Florentino Perez!” Mwaka Jana Ronaldo alikerwa na kuuzwa kwa Mesut Ozil kwa Arsenal na Breen-Turner ameeleza Ronaldo alimfuata Perez na kumueleza kuhusu kutofurahishwa kwake na safari hii pia Ronaldo alikwenda kumuona Rais huyo baada ya kuuzwa Di Maria.
Breen-Turner amedai, safari hii, Ronaldo alifuatana na Sergio Ramos kumwona Perez na kutaka Di Maria asiuzwe lakini hawakusikilizwa na hilo limemuudhi sana Ronaldo.
Breen-Turner ameeleza: “Hivi sasa Ronaldo hana furaha. Kitu kingine ni ule msimamo wake wa kila Siku kuisifia Man United na hivi Juzi kusifia sana kwa United kumsaini Falcao na kudai huo ni usajili kabambe. Kila kitu anachosema, kila kitu anachofanya ni kusafisha njia ya kurudi Man United!”

No comments:

Post a Comment