Pages

Thursday, September 11, 2014

NGUMI KUWAKA MOTO BAGAMOYO



                                                 September 11, 2014
Taarifa kwa vyombo vya habari

     Yah:- Mashindano ya ngumi ya wavuvi Boxing Tournament 13/09/2014
                                         Bagamoyo.

Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) limeaandaa mashindano ya ngumi ya wavuvi Boxing TOUNAMENT yatakayoanza kufanyika tarehe 13/09/2014 katika fukwe za Bagamoyo na baadaye kuendelea katika fukwe mbalimbali.
Lengo la mashindano hayo ni  kuhamasisha jamii ya wavuvi na watu wanaowazunguka kujishughurisha na masuala ya michezo na hasa mchezo wa ngumi baada ya shughuri zao za uvuvi na kuwafanya kuondokana na vitendo viovu vinavyotokana na utumiaji wa vilevi mbalimbali kupita kiasi na zaidi kuvumbua vipaji kutoka katika jamii hiyo ikiwa pamoja na kuwapa burudani.
Katika utafiti uliofanywa na BFT tumegunduwa kuwa katika jamii ya wavuvi wapo wengine wanaopenda michezo hasa mchezo wa ngumi hii ni kutokana na asili ya kazi yao ya uvuvi ya kutumia nguvu za mikono kwa ajili ya uvuvi na akili nyingi hivyo tumeazimia kuanza kuwafikia kwa vitendo kwa kufanya mashindano katika maeneo yao ili kuwahamasisha kijiingiza zaidi katika michezo.
Mashindano hayo yatakuwa yanafanyika kila siku ya jumamosi kwa fukwe mbalimbali za  bahari ya hindi na baadaye kuhamia katika fukwe za maziwa makuu.
Mashindano haya yamedhaminiwa na kampuni ya Sam & Anzai Boat Builder C.,Ltd kwa kushirikiana na  C&G
   
Makore Mashaga
Katibu mkuu.

No comments:

Post a Comment