Pages

Thursday, September 11, 2014

EL CLASICO YATHIBITISHWA NI OCTOBER 25, SUAREZ KUKUCHEZA AKITOKEA KIFUNGONI

Huko Spain wamethibitisha kuwa lile pambano kubwa Nchini humo lijulikanayo kama ‘EL CLASICO’, kati ya Vigogo na Mahasimu wakubwa, Real Madrid na FC Barcelona, itakuwa ni Jumamosi Oktoba 25 na hiyo inaweza kuwa ndio Mechi ya kwanza kabisa rasmi kwa Mchezaji mpya wa Barca Luis Suarez kucheza baada ya kumaliza Kifungo chake.
Suarez, ambae amehamia Barcelona kutoka Liverpool Mwezi Julai, alifungiwa na FIFA hapo Juni 25 kutocheza Soka kwa Miezi Minne kwa kukosa la kumuuma Meno Beki wa Italy Giorgio Chiellini wakati Uruguay inacheza na Italy Mechi ya Kombe la Dunia huko Brazil.

Kifungo cha Suarez kinakamilika Oktoba 24 na hivyo yuko huru kuichezea Barca hapo Oktoba 25 Uwanjani Santiago Bernabeu kwenye Mechi ya Kwanza ya La Liga kati ya Real Madrid na Barcelona.
Mechi hiyo itachezwa kuanzia Saa 1 Usiku, kwa muda wetu wa hapa Tanzania.
Luis SuarezLuis Suarez kwenye mazoezi na wenzake..Luis Suarez Wachezaji wa Barca wakifanya mazoezi na Luis SuarezLuis SuarezWakipeana neno na kufurahia jamboLuis SuarezLuis SuarezLuis Suarez
LA LIGA
RATIBA:
Ijumaa Septemba 12

22:00 UD Almeria v Cordoba
Jumamosi Septemba 13
17:00 FC Barcelona Athletic de Bilbao
19:00 Malaga CF v Levante
21:00 Real Madrid CF v Atletico de Madrid
23:00 Celta de Vigo v Real Sociedad
Jumapili Septemba 14
13:00 Rayo Vallecano v Elche CF
18:00 Valencia v RCD Espanyol
20:00 Sevilla FC v Getafe CF
22:00 Granada CF v Villarreal CF

Jumatatu Septemba 15
21:45 SD Eibar v Deportivo La Coruna

No comments:

Post a Comment