Pages

Tuesday, September 9, 2014

Lionel Messi amshinda Cristiano Ronaldo katika video game ya fifa ya kusaka wachezaji 15 bora


Cristiano Ronaldo alifanikiwa kumshinda Lionel Messi katika tuzo ya mchezaji bora wa dunia ya Ballon d'Or mapema mwaka huu, lakini mshambuliaji huyo wa Barcelona amelipiza kisasi kwa mshindani wake mkubwa wa kizazi cha sasa katika soka kupitia shindano lingine la FIFA la wachezaji bora 15 'video game'.
Akiwa amepata alama 93 kati ya 100, Messi ameongoza katika orodha ya mlinganisho wa ubora wa wachezaji kupitia mchezo wa video  (yaani video game)  wa shirikishp la soka duniani FIFA maarufu kama 'video game FIFA 15', ambao matokeo rasmi yanatarajiwa kutolewa septemba 26 nchini Uingereza.
Ili kuweza kumaliza ubishi kwa mashabiki watengenezaji wa mchezo huo kampuni ya EA Sports imeweka  orodha ya wachezaji 50 katika mchezo mpya kusaka wachezaji bora ambao wanaangaliwa kwa njia ya teknolojia ya video ambao utahusishwa watu wengi kuwezesha kutoa maoni yao.


Wanted man: Barcelona are sure to prove popular on the new game given Messi's eye catching statistics
Barcelona wana uhakika kupitia mchezo huu watu wengi watampa Messi kushinda
Real thing: The Argentine star (right) has started the season in typically impressive form for his club
Nyota wa Argentina(kulia) alianza msimu kwa kiwango cha kuvutia
Second best: Real Madrid's Cristiano Ronaldo has been given a rating of 92 on FIFA 15
Anayefuatia kwa ubora: Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amepewa 92 katika FIFA 15
Dangerous: EA Sports rate Ronaldo's shooting ability and pace at 93 out of 100
Hatari: EA Sports wamekadiria uwezo wa kupiga mpira wa Ronaldo na kupata kura 93 kati ya 100

Kubwa ambalo linazingatiwa katika kukadiria ubora wa mchezaji ni kwamba na hatimaye kutinga katika orodha ya wachezaji 15 bora kupitia shindano hili, inazingatiwa uwezo wako binafsi, uwezo wa kupiga mipira, kukokota mpita, idadi na upigaji wako wa pasi, kuzuia wapinzani na hata kufunga magoli.

ORODHA KAMILI FIFA 15 TOP 10 PLAYERS 

1. Lionel Messi 93
2. Cristiano Ronaldo 92
3. Arjen Robben 90
4. Zlatan Ibrahimovic 90
5. Manuel Neuer 90
6. Andres Iniesta 89
7. Luis Suarez 89
8. Bastian Schweinsteiger 88
9. Franck Ribery 88
10. Eden Hazard 88 

Katika orodha ya wachezaji 50 kuna idadi kubwa ya wachezaji kutoka katika klabu ya Bayern Munich ikiwa na jumla ya wachezaji 11, huku Real Madrid ikiwa na wachezaji 8.
Barcelona imeingiza wachezaji 6 akiwemo mchezaji bora wa mchezo huu mpya Lionel Messi.
Kwa upande wa klabu za Premier League Manchester United imeongoza ikiwa pia imeingiza wachezaji wake wapya Radamel Falcao na Angel Di Maria.
Kikosi cha Louis van Gaal jumla kimeingiza wachezaji 5 katika wachezaji 50 wakiwemo Juan Mata, Wayne Rooney na Robin van Persie.
Chelsea pia imeingiza wachezaji 5 akiwemo alisajiliwa kiangazi Diego Costa na Cesc Fabregas wakati ambapo Manchester City imeingiza wachezaji wanne tu kufuatia kuondoka kwa Jesus Navas.
Arsenal na Tottenham zote zimeingiza mchezaji mmoja kila moja Mesut Ozil na Hugo Lloris wakati ambapo Luis Suarez akiingia katika orodha hata baada ya kuihama Liverpool.

No comments:

Post a Comment