Pages

Saturday, September 6, 2014

LIGI DARAJA LA KWANZA (FDL) KUCHEZWA MAKUNDI MAWILI

Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/2015 itachezwa katika makundi mawili kwa mtindo wa nyumbani na ugenini kuanzia Oktoba 11 mwaka huu.

Kundi A lina timu za African Lyon, African Sports, Ashanti United, Friends Rangers, Kimondo SC, Kurugenzi Mafinga, Lipuli, Majimaji, Mlale JKT, Polisi Dar es Salaam, Tessema FC na Villa Squad.

Wakati kundi B lina timu za Burkina Faso, Geita Veterans SC, Green Warriors, Kanembwa JKT, Mwadui SC, Oljoro JKT, Panone FC, Polisi Dodoma, Polisi Mara, Polisi Tabora, Rhino Rangers na Toto Africans.

Ratiba ya Ligi hiyo itatolewa hivi punde.

No comments:

Post a Comment