Pages

Saturday, September 6, 2014

ISMAIL GUNDUZ, AFUNGIWA KUTOCHEZA MECHI 70 KAMA ADHABU YA KUMPIGA KICHWA MWAMUZI.

Mchezaji Ismail Gunduz wa SK Rum ya Austria amefungiwa kutocheza mechi 70 ikiwa ni adhabu baada ya mchezaji huyo kumpiga kichwa uwanjani mwamuzi wa mchezo.
Gunduz anayechezea timu ya daraja la tano ya SK RUM alimpiga mwamuzi siku ya Jumamosi kwa kichwa muda mfupi kabla ya mwamuzi huyo kupuliza kipyenga cha kumaliza mchezo.
Hata hivyo mwamuzi huyo alikimbizwa hospitali kwa matibabu kutokana na maumivu aliyoyapata baada ya kugongwa kichwa hicho.

Kwa mjibu wa sheria za soka za taifa hilo adhabu ya juu kwa kosa kama hilo ni kufungiwa michezo 108.

No comments:

Post a Comment