Pages

Friday, August 29, 2014

WAYNE ROONEYNAHODHA MPYA WA ENGLAND


KEPTENI wa Manchester United Wayne Rooney ndie ameteuliwa Nahodha mpya wa England na Meneja wa Timu Roy Hodgson.
Rooney, mwenye Miaka 28, anachukua wadhifa huo kutoka kwa Steven Gerrard wa Liverpool ambae amestaafu kuichezea England mara baada ya Nchi hiyo kutolewa hatua ya Makundi ya Fainali za Kombe la Dunia Mwezi Juni huko Brazil.
Rooney ameichezea England mara 95 na kufunga Bao 40 na Mwezi uliopita aliteuliwa kuwa Nahodha wa Manchester United na Meneja Louis van Gaal.
Mechi za kwanza kwa Rooney kama Nahodha wa England hapo Septemba 3 wakati England itacheza Mechi ya Kirafiki na Norway Uwanjani Wembley na kisha Septemba 8 kusafiri kwenda kucheza na Uswisi katika Mechi yao ya kwanza ya EURO 2016.
Mara baada ya kuteuliwa Rooney, Meneja Roy Hodgson alitangaza Kikosi chake cha England chenye Wachezaji wapya Wanne.
Wapya hao nI beki wa Arsenal mwenye Miaka 19, Calum Chambers, Mchezaji wa Newcastle Jack Colback, Danny Rose wa Tottenham na Fabian Delph wa Aston Villa, wote wakiwa na Umri wa Miaka 24.

KIKOSI CHA ENGLAND:
Makipa:
Fraser Forster (Southampton), Ben Foster (West Bromwich Albion), Joe Hart (Manchester City)
Mabeki: Leighton Baines (Everton), Gary Cahill (Chelsea), Calum Chambers (Arsenal), Phil Jagielka (Everton), Phil Jones (Manchester United), Danny Rose (Tottenham Hotspur), John Stones (Everton)
Viungo: Jack Colback (Newcastle United), Fabian Delph (Aston Villa), Jordan Henderson (Liverpool), James Milner (Manchester City), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal) Raheem Sterling (Liverpool), Andros Townsend (Tottenham Hotspur), Jack Wilshere (Arsenal)
Mafowadi: Rickie Lambert (Liverpool), Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge (Liverpool), Danny Welbeck (Manchester United)

No comments:

Post a Comment