Pages

Friday, August 29, 2014

OKWI ANAVYOCHEZA NA AKILI ZA VIONGOZI WA SIMBA


Emanuel Okwi wa Uganda ambaye msimu uliopita alikuwa anaichezea Yanga, akiwa na jezi namba 25 aliyokabidhiwa mara baada ya kusaini tena Simba baada ya kukachwa na Yanga katika usajili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayotarajia kuanza mwezi ujao.


Kamati ya usajili ya klabu Simba imetangaza kumsajili mshambuliaji wao wa zamani Emmanuel Okwi ambaye msimu uliopita alikuwa kwa mahasimu wao wa soka Yanga.

Akiongea mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo Zackaria Hans Poppe amesema wamemsajili Okwi baada ya mshambuliaji huyo raia wa Uganga kuomba kusajiliwa na klabu hiyo kufuatia kuvunjiwa mkataba na Yanga.

Poppe amesema mkataba wa Okwi na Simba ni wa wazi kwani mchezaji huyo ambaye amejiunga na Simba akiwa huru atakuwa huru kuondoka muda wowote atakapo taka kufanya hivyo.

Kwa upande wake Okwi amewataka wapenzi wa Simba kumchukuliwa yeye kama mchezaji mpya kwao na kwamba wasahau yaliyopita na wampokee kama mchezaji kijana mpya kwao
Kabla ya kujiunga na Yanga Okwi alikuwa akiichezea Sports Club Villa ya Uganda ambayo alijiunga nayo alitokea Etoile Du Sahel ya Tunisia ambako Okwi aliikimbia klabu hiyo kutokana na kile kilicho daiwa kuwa alinyimwa mshahara wake kwa zaidi ya miezi kinyume na makubalino ya mkataba.

Okwi anasajiliwa na Simba ikiwa siku mbili zimesalia kabla ya dirisha la usajili wa wachezaji wa ndani halijafungwa huku usajili wa wachezaji kutoka nje dirisha lake likitarajiwa kufungwa Septemba 6 2014

No comments:

Post a Comment