Pages

Thursday, August 28, 2014

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: ARSENAL 1 vs 0 BESIKTAS (Agg 1-0) ALEXIS SANCHEZ AIPA USHINDI GUNNERS EMIRATES.

Alexis Sanchez akishangilia bao lake.Alexis Sanchez aliipachia bao na kufanya 1-0 dhidi ya timu ya Uturuki Besiktas kwenye dakika za majeruhi za kipindi cha kwanza baada ya Jack Wilshere wa Arsenal kufanya jitihada na kumwachia afunge Sanchez aliyekuwa sehemu nzuri na kufunga bao hilo. Arsenal mpira huu hawakuumaliza 11 dakika ya 75 kipindi cha pili mchezaji wao Debuchy alipewa kadi ya njano ya pili na kuondoshwa kwa kadi nyekundu baada ya kufanya ndivyo sivyo.Patashika zikiendelea kipindi cha kwanza..Kimbiza kimbiza kila mchezaji akiunyatia kuupata mpira Jack Wilshere akisikitika baada ya kukosa bao huku akiwa kwenye nafasi nzuri katika dakika za mapema kipindi cha kwanza.Demba Ba (kulia) akiendesha.......Alexis Sanchez kuanza katika mchezo wao kati ya Arsenal vs Besiktas na hii ni baada ya kuumia kwa Olivier Giroud na sasa anarajiwa kuwemo katika mtanange huu wa leo  mchezo wa marudiano wa Champions League unaotarajiwa kupigwa punde usiku huu. Mechi ya kwanza walitoka 0-0 huko Uturuki.Podolski nae yumo...Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger
Kocha Mkuu wa England Roy Hodgson (akiwa nyuma) nae akishuhudia kipute kwenye Uwanja wa Arsenal Emirates.
VIKOSI:
Arsenal:
Szczesny, Debuchy, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Wilshere, Flamini, Oxlade-Chamberlain, Ozil, Cazorla, Sanchez.
Akiba: Martinez, Rosicky, Podolski, Chambers, Sanogo, Campbell, Coquelin.
Besiktas: Zengin, Koybasi, Franco, Gulum, Ramon, Hutchinson, Kavlak, Ozyakup, Pektemek, Sahan, Ba.
Akiba: Gonen, Kurtulus, Sivok, Tore, Uysal, Koyunlu, Tosun.
Refa: Pedro Proenca (Portugal)

No comments:

Post a Comment