Pages

Thursday, August 28, 2014

OLIVIER GIROUD NJE ARSENAL HADI MWAKANI

Straika wa Arsenal Olivier Giroud atakuwa nje ya Uwanja hadi baada ya Mwaka mpya kufuatia kufanyiwa upasuaji kutibu Mguu wake uliovunjika.
Mfaransa huyo mwenye Miaka 27 aliumia Jumamosi iliyopita huko Goodison Park wakati Arsenal inatoka Sare 2-2 na Everton kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.

Akitangaza habari hizi, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, alisema Giroud atakuwa nje kwa Miezi Mitatu hadi Minne.
Giroud alijiunga na Arsenal Mwaka 2012 kutokea Klabu ya France Montpellier na Msimu uliopita alianza Mechi 36 kati ya 38 za Ligi za Arsenal na kufunga Bao 16.
Licha ya pigo hili, Wenger ametangaza hatanunua Straika mwingine katika Kipindi hiki cha Dirisha la Uhamisho linalofungwa Septemba Mosi.

Arsenal sasa wamebakiwa na Mastraika Joel Campbell, Yaya Sanogo na Lukas Podolski lakini Mchezaji wao mpya, Alexis Sanchez, ambae kiasili ni Winga, huweza kucheza Sentafowadi na Jana Usiku ndie aliefunga Bao lilowapeleka Arsenal Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI wakati walipoipiga Besiktas Bao 1-0.

No comments:

Post a Comment