Pages

Saturday, August 23, 2014

ATLETICO MABINGWA SUPER CUP 2014 BAADA YA KUIFUNGA REAL MADRID 1-0 NA KUFUZU KWA (Agg 2-1), KOCHA SIMEONE NA LUKA MODRIC WAONESHWA RED CARD

Mario Mandzukic ndie aliyewapachikia bao la mapema na la ushindi dakika ya 2 Atletico Madrid nakufanya 1-0 kwenye mechi ya marudiano usiku huu baada ya kazi nzuri ya Antoine Griezmann. Kipindi cha pili timu zote mbili zilibanana na kutoshana nguvu ya bila kufungana licha ya kushambuliana mara kwa mara. zikiwa zimebaki dakika za nyongeza nne Luka Modric alioneshwa kadi ya njano ya pili na kutolewa nje kwa kadi nyekundu na mapema kipindi cha kwanza Kocha wa Atletico alitolewa nje ya Uwanja baada ya kutofautiana na Mwamuzi wa nje na hatimae kutolewa nje baada ya kukwaruzana na malalamiko ya mara kwa mara hapo kwenye wanja wao wa nyumbani Vicente Calderon.Mario Mandzukic akishangilia baada ya kufunga bao lake la mapema dakika ya 2 dhidi ya Real Madrid.Wachezaji wa Atletico wakipongezana..
Mapeeeeeeeeeeema Mario Mandzukic anaandika bao wakiwa kwao Vicente Calderon!Super CupWachezaji wa Atletico wakipongezana mbele ya Mashabiki wao

No comments:

Post a Comment