Pages

Friday, July 18, 2014

Wachezaji wa timu ya taifa ya Argentina watoa msaada hospitali ya tiba ya kansa jijini Buenos Aires.


Wachezaji wa timu ya taifa ya Argentina wamekubaliana kuchangia kiasi cha dola za kimarekani 135,000 katika hospitali inayotoa tiba ya magonjwa ya saratani huko mjini Buenos Aires.

Wachezaji wa taifa hilo ambao walicheza hatua ya fainali kwenye michuano ya kombe la dunia, na kukubali kufungwa bao moja kwa sifuri dhidi ya Ujerumani wamewasilisha mchango huo kwenye hospitali ya Garrahan wakiongozwa na nahodha na mshambuliaji wao Lionel Messi.
Hospitali ya tiba za kansa nchini Argentina
Kwa makusudi ya dhati wachezaji wa Argentina walikubaliana kwa pamoja kuwasilisha mchango huo ambao unatokana na zawadi ya dola za kimerakani million 25, ambazo wamekabidhiwa na FIFA baada ya kushika nafasi ya pili kwenye fainali za kombe la dunia za mwaka huu.

Katika ujumbe wa pamoja na wachezaji hao imeonekana kuguswa na mahitaji ya hospitali hiyo, ambayo kila leo hutoa huduma kwa wagonjwa wa saratani, hivyo wanaamini mchango wao utasaidia kukidhi baadhi ya mambo hospitalini hapo.

No comments:

Post a Comment