Pages

Saturday, July 5, 2014

RYAN GIGGS ALA NONDOZZ....AWA DAKTARI WA SAYANSI BOLTON


Gwiji wa Manchester United akipozi katika picha baada ya kupata digrii yake kwenye ukumbi wa Victoria Hall mjini Bolton.
Aliyekuwa Kocha wa Muda wa Manchester United Ryan Giggs, amezawadia shahada ya heshima ya Udaktari na chuo kikuu cha Bolton kutokana na mchango wake mkubwa aliotoa katika mchezo wa soka.
Giggs aliyestaafu kucheza soka mwishoni mwa msimu uliopita amepokea udaktari wa sayansi kwa mchango wake mkubwa katika michezo kwenye mahafali ya chuo iliyofanyika ukumbi wa Victoria Hall mjini Bolton jana ijumaa mchana.
Giggs anaongeza shahada hiyo katika shahada yake ya kwanza ya OBE aliyopata kutoka kwa Malkia mwaka 2007, shahada ya pili (MA) alipewa mwaka uliofuata na chuo cha Salford.


Giggs aliwapongeza wanafunzi wa chuo kwa kupata digrii zao.

No comments:

Post a Comment