Kilio cha mtu mzima: Liuz akibubujikwa na machozi baada ya kichapo cha maangamizi kutoka kwa Ujerumani |
Nahodha wa muda wa Brazil David Luiz amewataka
mashabiki wa timu hiyo kote duniani kuwasamehe wachezaji waliokuwa
uwanjani Selecao ilipoadhibiwa kichapo cha mabao 7-1 na Ujerumani
katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la dunia huko Brazil.
Amini Usiamini Ujerumani ilikuwa inaongoza mabao 5-0 kufikia dakika 29 ya kipindi cha kwanza .
"Wajerumani walikuwa timu bora zaidi yetu''
Luiz,ambaye alitajwa kama nahodha wa muda
baada ya marufuku ya Nahodha Thiago Silva kumlazimu kutizama tu mechi
hiyo alisema hawjui kilichotendeka lakini ni wakati wao kujifunza
kutokana na aibu hiyo ya kusakamwa 7-1. "Ni siku ya majonzi tele kwa
wabrazil''.
"Mtuwieni radhi sijui tutafanya nini ilituwaone tena wabrazil wakitabasamu,?
Kilio kimezidi kote nchini humo haswa baada ya
nyota wa Brazil Neymar kujeruhiwa uti wa mgongo Ijumaa iliyopita katika
mechi ya kufuzu kwa nusu fainali dhidi ya Colombia.
Kwa Upande wake Kipa wa Brazil Julio Cesar alitaja dakika hizo kumi timu hiyo ilipofungwa mabao manne kuwa sawa na kuzimia.
''Sio jambo unaloweza kujieleza.
Kombe hili la dunia limekuwa lenye ufanisi hadi leo.
Hata hivyo tunawashukuru Wabrazil kwa kutuunga mkono katika kipindi hichi chote .
Hata wachezaji wakiomba msamaha kwa kichapo hichi cha leo,ni wazi kuwa mjerumani alituzidi maarifa .
Lazima tukubali hilo walikuwa bora kutuzidi leo.'''
No comments:
Post a Comment