Samuel Eto’o kuelekea Italia |
KLABU ya AS Roma ya Italia imeanza
mazungumzo na wawakilishi wa Samuel Eto’o jana ikiwa ni baada ya kukamilisha
usajili wa mchezaji mwenzake wa zamani wa Chelsea Ashley Cole.
Eto’o
mwenye umri wa miaka 33 ni mchezaji huru toka aondoke Stamford Bridge na
tayari amepata ofa kutoka China na Uturuki lakini mwenyewe anataka
kurejea nchini Italia.
Katika mazungumzo hayo nyota huyo anatarajiwa
kupunguziwa mshahara wake kwa kiasi cha paundi milioni tatu ikiwemo na
posho.
Kama akifanikiwa kutua Roma atakuwa amejiunga na mchezaji
mwenzake kutoka Chelsea, Cole aliyesaini mkataba wa miaka miwili na timu
hiyo huku ikiwa ni mara ya pili kwa nyota huyo kurejea nchini Italia
baada ya kuitumikia Inter Milan kati mwaka 2009 na 2011.
No comments:
Post a Comment