Pages

Thursday, July 31, 2014

MSHAMBULIAJI WA CHELSEA ROMELU LUKAKU ATUA EVERTON KWA DAU LA PAUNDI MILIONI 24

Msimu uliopita, Lukaku alifunga mabao 15 akiwa na klabu ya Everton ambayo inakaribia kumsajili kwa mkataba wa kudumu.
Romelu Lukaku atakamilisha uhamisho wa kujiunga na Everton kwa dau la paundi milioni 24 baada ya kutangaza kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twita mchana wa leo akisema: Ni muda wa kuanza ukurasa mpya.Striker: Lukaku will wear the number 10 shirt at Goodison Park this season
Inafahamika kuwa nyota huyo mwenye miaka 21, ambaye msimu uliopita alikipiga Goodison Park kwa mkopo atasaini mkataba wa miaka mitano na Everton na kuvunja rekodi ya usajili ya klabu hiyo.Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji aliyeiwakilisha nchi yake katika fainali za mwaka huu za kombe la dunia nchini Brazil, amekuwa akihusishwa kuondoka darajani majira yote ya kiangazi mwaka huu.Everton ameamua kumpa mkataba wa kudumu baada ya kuwa na rekodi nzuri ya kufunga mabao 15 msimu uliopita.
Record: Romelu Lukaku (left) has signed for Everton for £28million from ChelseaRoberto Martinez ameamua kuvunja rekodi ya dau la usajili la klabu ambapo dau alilosajiliwa Marouane Fellaini la paundi milioni 15 lililokuwa linashikilia rekodi.Nafasi ya Lukaku katika klabu yake ya Chelsea ingefinywa zaidi na Diego Costa, Fernando Torres na Didier Drogba aliyesajiliwa siku za karibuni.Hii ni taarifa njema kwa mashabiki wa Eberton ambao jana walimshuhudia Ross Barkley akijifunga mkataba wa miaka minne Goodison Park.

Kocha wa  Everton Roberto Martinez akimsifia  Lukaku mbele ya Waandishi wa Habari na kudai kuwa Lukaku ataonesha picha wapi wanaelekea zaidi..

Lukaku aliwachezea Everton kwa mkopo msimu uliopita na kufunga mabao kadhaa

 Romelu Lukaku moja kwa moja alinaswa kwa  £28million kutoka  Chelsea

 Lukakuna meneja wake  Roberto Martinez

Matabasamu ya nguvu: Lukaku kwenye ukumbi wa Habari

Romelu Lukaku ameweka Historia kusajiliwa na Everton kwa kiasi hicho na akitokea Chelsea....

No comments:

Post a Comment