Pages

Thursday, July 31, 2014

MIEMBENI FC WATINGA FAINALI BAADA YA KUIFUNGA BAO 2-1 BILELE FC KWA DAKIKA 120!


Wachezaji wa timu zote mbili Miembeni Fc na Bilele Fc  wakisalimiana kabla ya Mtanange kuanza jioni hii.
Kikosi cha Timu ya Miembeni Fc
Kikosi cha Timu ya Bilele Fc
Mabingwa watetezi wa kombe la KAGASHEKI, Bilele Fc, wamefungwa leo na Timu ya Miembeni Fc bao 2-1 kwenye mtanange uliopigwa dakika 120, Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kwa  kutoshana nguvu kwa bao 1-1.
Timu ya Bilele Fc ndio walianza kupata bao la mkwaju wa penati katika dakika ya 62 kupitia kwa Fikiri David na Miembeni Fc wakasawazisha bao hilo ndani ya dakika moja na Rashid Mandawa kupita katika dakika 63 baada ya mpira kuanza kati na kufanya shambulizi.
Dakika 90 zilimalizika na kwenda katika dakika za ziada na katika dakika ya 105 Miembeni walifanikiwa kupata bao la ushindi na mtanange kumalizika. Mtanange huu pia haukuweza kumalizika vyema kwani wachezaji wawili wa Miembeni Fc wameoneshwa kadi nyekundu 2 na kucheza pungufu katika dakika za mwishoni kwa kufanya makosa tofauti tofauti.
Ushindi huu unawapeleka  Miembeni Fc  hatua ya Fainali wakisubiri mshindi wa kesho kati ya Kitendaguro Fc na Kagondo Fc.
Bilele Fc wao wanasubiri atakayefungwa kesho kati ya Kitendaguro na Kagondo ili waje wakutane kutafuta mshindi wa tatu.Fikiri David wa timu ya Bilele Fc akimfunga kipawa Miembeni Samwel Geofrey kwa Mkwaju wa penati katika kipindi cha pili dakika ya 62.Fikiri David akishangilia bao lake mbele ya Mashabiki wao Nao Miembeni hawakupoteza nafasi walisawazisha bao hilo  ndani ya dakika chache moja na kufanya 1-1 katika kipindi hicho cha pili, Bao likifungwa na Rashid Mandawa.Kipa wa Miembeni akipangua mpira uliopigwa kwa kona.Wachezaji wa Bilele fc wakimdhibiti mchezaji wa Miembeni.Jesse Johansen wa Miembeni Fc akimkimbiza mchezaji wa Bilele fc Mohamed Nunda Mchezaji wa Miembeni Babu Seif (kushoto) akimtoka mchezaji wa Bilele fcKipa wa Miembeni fc Samwel akiwapanga wachezaji wake Frii kiki kuelekea lango la Miembeni fcKipa wa Miembeni Samwel Geofrey aliumia katika kipindi cha pili na mpira kusimama kwa mudaKipa wa Miembeni Samwel Geofrey akisimama na kuendelea kulinda lango lakePatashika langoni mwa timu ya Bilele FcKipa wa Miembeni samweli Geofrey akiokoa mpira wa kona langoni mwake Kipindi cha dakika za ziada 120 wachezaji wa Miembeni waliboresha ngome yao ili kulinda bao lao na hatimaye kuibuka na ushindi.Mashabiki wa Miembeni Fc wakishangilia baada ya kuibuka na ushindi wa bao 2-1 na kwenda hatua ya Fainali

No comments:

Post a Comment