Muonekano wa nje wa uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi |
Uwanja
wa Azam Complex uliko Chamazi jijini Dar es Salaam unakuwa uwanja wa
kwanza kwa upande wa Tanzania Bara kutumika kwa michezo ya ligi kuu ya
soka nyakati za usiku.
Akiongea
na mtandao huu wa Rockersports, mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Silas
Mwakibinga amesema kuwa uwanja huo kwasasa unafungwa taa maalumu za
kuruhusu mwanga wa kutosha wakati mchezo huku lengo kuu la matumizi ya
uwanja huo usiku ikiwa ni kuifanya ratiba ya ligi kuu kwenda na wakati
na kumalizika kwa wakati.
Mwakibinga
amesema ratiba ya ligi hiyo msimu huu imezingatia mambo mbalimbali kwa
lengo la kuifanya kuwa rafiki zaidi akitolea mfano wa kuipishanisha na
ratiba ya michezo ya ligi kubwa barani Ulaya ambayo michezo yake mingi
mikubwa ilikuwa ikifungana na michezo yenye mvuto kwa hapa nchini na
hivyo kupunguza watazamaji wa uwanjani ambao wanafafuatilia ligi za
Ulaya na kuathiri mapato ya milangoni.
Uwanja utatumika kwa michezo ya ligi ya ligi kuu nyakati usiku |
Amesema
kwa kuzingati hayo na mengine yanayofanana na hayo Bodi yake imeonelea
ni vema kufanya mazungumzo na uongozi wa Azam fc ili kuona kama kuna
uwezekanao wa kuruhusu michezo mingine ya ligi hiyo kupigwa usiku kwenye
uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi jambo ambalo kimsingi
limekubalika na sasa mchakato wa uwekaji taa maalumu za viwanjani
unaendelea.
Hii
inakuwa ni historia kwa ligi kuu ya soka ya Tanzania bara kuchezwa
usiku kwa mara ya kwanza tofauti na Zanziba ambako uwanja wa Amani
umekuwa ukitumika kwa michezo yake ya ligi kupigwa nyakati hizo.
Kumbuka
kuwa uwanja huo umeshatengeneza historia ya kwanza kuwa uwanja wa
kwanza unaomilikiwa na klabu nchini Tanzania kuruhusiwa na shirikisho la
soka barani Afrika CAF kutumika kwa michezo ya kimataifa ya ngazi za
vilabu.
Hiyo
ilifuatia jitihada za uongozi wa klabu ya Azam fc ambao ndio klabu
bingwa nchini Tanzania kuomba CAF kuwaruhusu michezo yao ya klabu
bingwa Afrika kufanyika uwanjani hapo.
Kumbuka
Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara inatarajia kuanza kutimua vumbi Septemba
20 mwaka kufuatia kusogezwa mbele kutoka Agosti 24 kwasababu zilizo
elezwa na TFF za kupisha michezo ya kimataifa ya vilabu na timu ya
Taifa.
No comments:
Post a Comment