Pages

Monday, July 28, 2014

BONDIA SELEMANI KIDUNDA WA TANZANIA APOTEZA MCHEZO JUMUIYA YA MADOLA


Selemani Kidunda
Bondia Selemani Kidunda amepoteza mchezo wake dhidi ya bondia kutoka nchini Nigeria Kehinde Ademuyiyiwa uzito wa kilo 69 na hivyo kupoteza nafasi ya kusonga katika hatua inayofuata katika michezo ya jumuiya ya Madola inayofanyika Glasgow nchini Scotland.
Akiongea na mtandao wa rockersports kocha mzalendo wa timu ya ngumi John Mwakipesile amesema mchezo ulikuwa ni mzuri kwa upende wa Kidunda kwa roundi zote tatu za mchezo na mpaka kufikia mwisho walikuwa wakijua Kidunda ameshinda lakini ikawa ni ajabu kwa watu wengi kutangazwa Ademuyiyiwa kutangazwa mshindi.
Amesema mpianzani wake alikuwa akitumia mbinu chafu ya kumpiga vichwa Kidunda katika sehemu kubwa ya mchezo huo kitu ambacho waamuzi wa mchezo walikuwa wakikiona na kushindwa kukemea hilo.
Kuondolewa kwa Kidunda ni pigo kubwa kwa Tanzania ambayo ilikuwa imeweka matumaini makubwa kwa nahodha huyo wa Tanzania katika michezo hiyo ya Madola.
Kesho bondia mwingine Nasser Mafuru atapanda ulingoni kucheza dhidi ya Jessie Lartey wa Ghana ambapo mwenye Mafuru ametamba kumchapa mpinzani wake huyo.

No comments:

Post a Comment