Lakini bado kidogo waukose ushindi huu muhimu kwani waliongoza 2-0 hadi Mapumziko na City kujitutumua Kipindi cha Pili na kusawazisha na Gemu kuwa 2-2 na ndipo ikaja zawadi kwa Liverpool kutoka kwa Nahodha wa City, Vincent Kompany, ambae aliokoa fyongo na Mpira ukamkuta Phillippe Coutinho alieachia Shuti tamu na kuwapa Bao la ushindi.
Man City walipata pigo kwenye Dakika ya 19 wakati Kiungo wao mahiri, Yaya Toure, alipolazimika kutoka baada ya kuumia Goti na nafasi yake kuchukuliwa na Garcia.
Dakika ya 93 Kiungo wa Liverpool Henderson alipewa Kadi Nyekundu na Refa Mark Clattenburg kwa Rafu mbaya aliyomfanyia Samir Nasri.
Ushindi huu umewabakiza Liverpool kileleni wakiwa na Pointi 77 kwa Mechi 34 wakifuatiwa na Chelsea, ambao watacheza baadae Leo, wakiwa na Pointi 72 kwa Mechi 33 na City kukamata Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 70 kwa Mechi 32.
No comments:
Post a Comment